Watengenezaji Vitumaji Ujumbe Wanapaswa Kufanya Nini?

Katika mojawapo ya machapisho yetu ya hapo awali tuliuliza swali: mtumiaji anahitaji kitumaji ujumbe kipi? Sasa baada ya ya kufanyia utafiti machaguo yote yaliyopo ni wakati wa kuorodhesha mahitaji yote makuu kwa njia ya usahihi zaidi.

 1. Huduma hii ni lazima isiwe na fursa ya kiufundi ya kutuma kitu chochote baada ya ombi kutoka kwa wawakilishi rasmi wa taifa, na pia kutoka kwa mtu na mashiriki mengine yoyote. Hakuna data ya mtumiaji inapaswa kuhifadhiwa kwenye seva za kitumaji ujumbe.
 2. Data zilizohifadhiwa kwenye vifaa vya watumiaji – zote, pamoja na ujumbe wa sauti na video, picha ni lazima zisimbwe papo hapo kulingana na viwango vya hivi sasa zaidi.
 3. Ni lazima mtumiaji awe na chaguo la kiwango cha usalama wa programu anayotumia: usalama kamili pamoja na vikwazo vinavyoonekana katika urahisi wa kutumia; au utendaji kamili pamoja na maelewano maalum kuhusu ufikiaji data za kibinafsi (kama katika tukio la uchukuaji kifaa bila amri).
 4. Mtumiaji ni lazima apewe chaguo la kujisajili akitumia jina la utani:
 • nambari ya simu ya kibinafsi;
 • barua pepe;
 • na, pia, jina la utani.
 1. Ni lazima mtumiaji awe na hakikisho kwamba jina lake halitafichuliwa kamwe na ana haki kamili ya kumzuia mtumiaji yeyote. Kuanzisha mazungumzo na mtumiaji huu, kubadilishana maelezo yoyote kunawezekana tu baada ya ruhusa yake ya moja kwa moja.
 2. Msimbo wa utengenzaji ni lazima uwe wazi. Protokali na msimbo ni lazima zipatikane ili wataalam wanaojulikana vyema waweze kuufanyia utafiti wa mara kwa mara na huru. Timu ya mradi inapaswa kuchapisha matokeo ya kitaalamu hata kama hawakubaliani nayo. Katika sehemu hii kipengele muhimu kimkakati ni kutoficha data zinazoweza kujadiliwa bali ni kufanya majadiliano ya kijamii ambayo hatimaye yatapelekea hali halisi ya matukio[1].
 3. Makosa yote muhimu ambayo watumiaji wanaripoti ni lazima yakubalike hadharani na kusuluhishwa haraka iwezekanavyo kadri ya uwezo wa mradi. Wawakilihsi wa huduma wana jukumu la kuhsiriki katika majadiliano ya hadharani, na kuzungumza kwa niaba ya timu.
 4. Wawakilishi wa huduma wana jukumu la kuchapisha data kuhusu maombi kutoka kwa mamlaka ambayo yanahusiana na data za wateja ndani ya mamlaka ambazo zinaruhusu hili.
 5. Huduma hiyo ni lazima impe mtumiaji zana fanisi dhidi ya ujumbe wowowote taka.
 6. Huduma ni lazima itaje vyanzo vyake vya kifedha.

Kwa hivyo, orodha hii ya vipengele kumi imetusaidia kujua kitumaji ujumbe bora zaidi – huduma ya kuotewa ambayo kwa sasa haipatikani. Hali hizi zinaonekana kuwa za kustaajabisha tukizingatia kwamba kuna mamia ya programu za kutuma/kupokea ujumbe papo hapo. Miongoni mwa hizo kuna programu ambazo zinageuka na kuwa mitandao ya kijaa, nyingine zinakuwa programu za huduma za benki; nyingine zinageuka kuwa mikutano ya wataamu, nyingine zinaunda ‘teknolojia ya kipekee ya ulinzi’ ambayo ina ‘kiwango cha usimbaji sawia na cha jeshi’ na kadhalika.

Ingawa zote hazijatekeleza mchanganyiko rahisi na nadra wa fursa msingi: kuhifadhi data zote za mtumiaji kwenye kifaa cha mtumiaji kwa kiwango bila kikomo kwa kipindi chote cha kutumia huduma na data hiyo kutofikika na wahusika wengine ikijumuisha hali za maabara.

Pengo hili katika soko lililosongamana la mawasiliano mengi lina sababu rahisi: kutengeneza programu hiyo kunahitaji rasilimali nyingi na kila wakati si pesa zinazoweza kusuluhisha tatizo kama hilo. Kuna wataalamu wachache zaidi ambao wako tayari kufanyia kazi mradi kama huu mgumu, mzito na mkubwa kiasi hiki. Kuwaunganisha watengenezaji programu na mameneja bora katika timu moja ni jambo hata nadra zaidi.

Na hata wakati bidhaa kama hii inapotengenezwa ni lazima iingie soko la ulimwengi ambapo hakuna mtu anayeisubiri. Jambo hili la ‘hakuna mtu’ linaungwa mkono na tatizo sugu zaidi: maelefu na hata mamilioni ya mipango ilitokomea baada ya watengenezaji wake kukosa kukagua mahitaji ya soko na mitazamo ya mradi. Ni jambo la kweli: mkutano wa kwanza na mwekezaji, simulizi kuhusu siku nzuri zijazo zilizo za dhana hii na jibu linatolewa: hakuna mtu anayeihitaji, haifanya vyema!

Na ndio sababu makala ya mwisho ya msururu wa kwanza tutakueleza kuhusu wale ambao kwa kweli wanahitaji kitumaji ujumbe kilichosimbwa.

[1] Mfano mzuri unaweza kuwa chapisho kuu katika jarida la The Guardian, ambapo mtafiti anayejulikana vyema alizungumza kuhusu mlango wa nyuma uliopo katika WhatsApp. Mjadala zaidi na viongozi bora katika sekta ulisaidia kuongeza sifa kwenye huduma hii.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Jisajili Kupokea Jarida Letu

Kitumaji Ujumbe cha Aegees cha 2018. Haki zote zimehifadhiwa.