Viber nzuri kweli kweli

Tukitathmini mikakati ya utangazaji, basi Viber ni kinyume kabisa na Telegram: ni kitumji ujumbe ambacho mara nyingi kinarejelewa kama ya Kibelarusi. Toleo hili liliungwa mkono katika ngazi ya juu: mwezi Januaru 2017 Raisa wa Belarusi alisema kwamba programu hii ni tokeo la watengenezaji Wabelarusi. Kwa sehemu fulani hajakosea kwani mmoja wa waanzilishi wa mradi huu ametoka nchi hii na kando na hilo kuna ofisi mbili za kampuni hii zilizoko nchini humo. Timu nyingine ya IT inafanya kazi ikiwa nchini Israeli na makao yake makuu yamo nchini Laksenibagi. Na mmiliki wa huduma hii ni Kampuni ya Kijapani inayoitwa Rakuten.

Hata hivyo, hatuna haja na asili wala mikakati ya kutengeneza taswira ya kampuni – haja yetu ni kuhusu usalama wa bidhaa hii. Kwa mtazamo wa kwanza sehemu hii inaonekana kuwa ya kawaida: historia ya ujumbe inahifadhiwa wazi kwenye vifaa vya watumiaji, usimbaji kwenye upande wa kutuma na kupokea na utekelezaji wa protokali yake binasfi inayoitwa Proteus (kimsingi sawia na Signal).

 

kiungo kuelekea kwenye video ya nne

Mwezi Aprili 2016 wawakilishi wa kampuni walisema:

Viber haitapatiana historia ya ujumbe katika nchi yoyote wala katika hali yoyote ile. Tuna msimamo sawia na Apple na WhatsApp. Kampuni una rekodi ya mawasiliano baina ya nambari tofauti za simu, lakini hatuna maudhui ya ujumbe wenyewe wala mazungumzo yenyewe.

Hili ni jambo nzuri lakini hebu tuangazia hali ilivyo. Viber imepigwa marufuku, tuseme, nchini China – hilo si jambo la kushangaza kwani intaneti nzima inadhibitiwa nchini humo. Huduma maarufu za VoIP kama vile Viber, Skype na WhatsApp zimepigwa marufuku nchini Saudia tangu mwaka 2013 na hilo limepelekewa na nia kinzani za watoa huduma wa ndani. Kumetajwa majaribio ya kuwekewa vikwazo katika nyingine (ikiwemo Belorusia) na hilo pia limepelekewa na usalama wa watoa huduma katika ngazi ya kitaifa.

Hakuna data nyingine zinaonyesha kitumaji ujumbe hiki kikiwa na mgogoro na mamlaka. Kila mtu yuko sawa na Viber.

Wakati huo huo huduma hiyo iko hatarini mwa mashambulizi mbalimbali: kwa mfano, inatosha kufungua picha iliyotumwa na mhalifu. Mwezi Januari 2017 wataalam wa Kirusi walichapisha data kuhusu mawasiliano kudukuliwa kupitia kitumaji ujumbe hiki kwenye vifaa tamba. Aidha wajati wowote mtumiaji anapotuma picha, michoro au kushiriki mahali alipo maelezo haya kwa urahisi yanaweza kuchukuliwa na mtu aliye katikati.

Lakini sababu ya kuwepo kwa chapisho la kando kuhusu Viber ni kwa ajili ya utafiti maizi wa kiufundi. Ili kuelezea tatizo kuu la kitumaji ujumbe hiki kwa maneno hakuna haja ya kutegemea mani ya mtaalami wala kufanya majaribio ya maabarani. Mambo ni ya kawaida zaidi…

Programu kutoka kwa vitumaji ujumbe 5 maarufu zaidi duniani[1] ni kiongozi katika idadi ya ujumbe taka. Haitoshi kusema tu kwambaa ni nyingi kupindukia. Ni jambo mbove zaidi kwamba watumiaji hawawezi kuchuja ujumbe kutoka kwa watoa huduma na wauzaji ambao wamepigwa marufuku na sheria. ‘Kitumaji ujumbe cha akina mama wa nyumbani’ ambao hakina madhara kinatumiwa na walaguzi madawa ya kulevya, wafanyabiashara ya ukahaba na wawakilishi wengine wa ulimwengu wa jinai.

Na huo si mwisho wake: huduma hii yenyewe haionekani ‘kustaarabika’ kama inavyodhaniwa. Viber hukusanya data nyingi iwezekanavyo kumhusu mtumiaji, haswa kupitia matoleo ya kompyuta. Na hata haiijaribu kuficha hili – inatangaza sera yake hadharani.

[1] Bila kujumuisha vitumaji ujumbe vya Kichina WeChat na QQ kwenye orodha ya kadirio.

 

Nao watumiaji hawafichi hisia zao wanapotathmini huduma hii. Hapa ni maoni ya kawaida zaidi yaliyopatikana mtandaoni:

“…jambo la kuhuzunisha zaidi ni kwamba picha zako zote unazotuma kwa rafiki zinakuwa za kupatikana hadharani. Hakuna sera yoyote ya usiri. Wasiliani wako wala ujumbe wako wa maandishi, wala picha au video hazipo salama. Kila kitu kinaingia kwenye chungu kimoja kinacoweza kufikiwa na kila mtu…”

“Na hakuna njia ya kuzuia taka hizi, hata ukiizuia bado kuna ujumbe unaotokea unaoniuliza kama bado ningependa kuzisoma…”

“Viber yangu imedukuliwa ingawa hakuna mtu amewahi kugusa simu yangu. Na sasa kwa kutumia jina langu kuna kundi limeundwa na baadhi ya bidhaa zinauzwa. Tafadhali nieleze ninachoweza kufanya?”

“Hivi majuzi tuligundua kutoka kwa marafiki wetu kwamba nambari ambayo mke wangu anatumia kupiga simu pekee imetokea kwenye Viber. Na picha yake inashinda ikibadilika badilika na kuonyesha maudhui ya utangazaji <…> na ninapotuma ujumbe wa viber kwa nambari hii, mtu wangu hapokei ujumbe huo kwenye simu yake na hakuna anayejibu. Baada ya kujaribu kubadilisha sim-kadi, kuweka simu upya, kubadilisha akaunti jhakuna kinachosaidiana programu dhidi ya virusi haigundui virusi vyovyote vile. Jambo kuu hapa ni kwamba hauwezi kuingia kwenye viber ukitumia nambari hii iwe ni kwenye simu yako, wala kwenye kompyuta yako…”

“hiyo ni kuwa na hifadhidata iliyojaa nambari (nambari kadhaa zinazofuatana) na baada ya kuzingeza katika wasiliani mtu anweza kuziweka pamoja na kusambaza ujumbe taka. Hilo ndilo wao hufanya”.

Kuweka hitimisho, mtu anaweza kusema kwa uhakika kwamba usalama wa Viber ni mchache zaidi kuliko inavyodaiwa. Kasoro zake ni mfano mzuri wa mbinu ya mbaya ya kutekeleza bidhaa: watengenezaji huduma hii wameshughulikia usimbaji, kutangaza wanaheshimu haki na uhuru wa umma… na kutelekeza hali kuu ya wateja wao kwa kuwageuza kuwa chombo cha uchumaji pesa bila huruma.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Jisajili Kupokea Jarida Letu

Kitumaji Ujumbe cha Aegees cha 2018. Haki zote zimehifadhiwa.