Unapatikana kwa ajili yangu, lakini sipatikani kwa ajili yako.

Hebu tujibu swali lililoulizwa mwishoni mwa chapisho la kwanza la msururu huu: la, hatutaki kutuma data zetu za kibinafsi kwa mhusika mwingine, yeyote yule. Hebu tutazame ni wakati gani huduma za kutuma na kupokea ujumbe zinaweza kuaminika katika tukio hili.

Kwanza hebu tufafanue vigezo msingi vya ukaguzi: ni lazima tujue haswa hali ya mfumo wa kufadhili huduma ambayo tunataka kutumia: uwekezaji, kuchangisha fedha, ruzuku. Na pia utekelezaji wa ulinzi (au njia za usimbaji) uliotangazwa na timu. Ukaguzi wa wataalamu huru kuhusiana na matokeo ya ukaguzi wa msimbo na usalama pia huenda ukawa muhimu.

Hebu tutazame bidhaa maarifu zaidi.

Ya kwanza kwenye orodha yetu ni kitumaji ujumbe kizuri na thabiti cha Signal ambayo ilifanyiwa promosheni na mtaalamu ‘gwiji’ mwanzoni kabisa na baadaye – ilipata sifa nzuri katika vyombo vya habari.

Signal ni ya msimbo unaopatikana wazi, na hufanya kazi kwenye protokali yake binafsi ambayo ilitambulika bila kupingwa miongoni mwa viongozi kwenye sekta hii (protokali sawia inatumia na Facebook Messenger, Google Allo, Skype, WhatsApp). Huduma hii ipo kutokana na fedha kutoka kwa wajitoleaji na ruzuku kutoka kwa mashirika ya kijamii. Kando na hilo kumetajwa usaidizi kutoka kwa timu za utengenezaji za baadhi ya taasisi za kiserikali.

Laki, lo, hapa pia tutapata kero; majaribio yoyote ya kutaka kujua ni mifumo ipi ya serikali na kwa kiwango kipi ilivyohusika hayajafua dafu. Watengenezaji kitumaji ujumbe hiki hawafichui data zozote kuhusu kiwango cha ufadhili au masharti ya ufadhili huo.

Hitimisho: huenda Signal si thabiti kama inavyotaka kuonyesha. Au timu hiyo haithamini sifa yake nzuri ambayo kwa sasa ni nzuri sana. Tunaweza kusema kwa kweli kwamba tuhuma za watumiaji kuhusu ushirikiano baina ya Signal na serikali hazijawahi kupingwa na timu.

Kama tunavyoona msimbo wa utengenezaji unaopatikana wazi na matangazo mazuri hayahakikishii ulinzi wa data zetu endapo nia kutoka kwa upande wa serikali itaibuka. Hata hivyo, kinyume chake ni kweli pia.

Bidhaa nyingine maarufu – kitumaji ujumbe cha Skype – ambayo ina watumiaji wengi na usaidizi wa kiufundi kutoka kwa kampuni kubwa katika sekta – hapa kila kitu kinaonekana kuwa sawa. Mfumo wa kutengeneza pesa upo thabiti, protokali inayotumika imelindwa vyema, mmiliki anajulikana vyema. Hata hivyo hata hadithi hii ya mafanikio ina hitilafu ambazo ni gumu kuzitambua latiki bado ni muhimu.

Kila wakati Skype husema ‘ndiyo’ wakati serikali inapoiombe ifichue data za mtumiaji. Hatujawahi sikia kwamba imesema ‘la’ inapopopokea ombi kama hilo. Kando na hilo huduma hii kwa mara zaidi ya moja imetuma misimbo yote ya utengenezaji wa programu hii kwa huduma za usalama za serikali na kuwaruhusu kudhibiti maelelzo yote yanayotumwa.

Mfano wa hivi majuzi zaidi: katika mwaka 2017 mmoja wa wataalam wa usalama waligundua hatari mbaya zaidi katika toleo la kompyuta la Skype ambapo inaruhusu kupata udhibiti kamili wa kompyuta inayoshambuliwa. Kma jibu kwa makala hayo wawakilishi wa kitumaji ujumbe hiki walisema kwamba tatizo hilo lipo na wanalifahamu lakini – makinika! – hawatalirekebisha kwa sababu sehemu kubwa sana ya msimbo itahitajika kuandikwa upya’.

Hebu tukalimani haya kwa lugha ya kawaida: kwetu kila kitu kipo sawa, hakuna chochote kinachozuia utengenzaji pesa.

Mfano wa tatu huenda ukawa wakueleweka zaidi. Unahusu kampuni mbili kubwa katika sekta, moja ni WhatsApp ambayo ni maarufu kote ulimwenguni. Jan Kuom, mwazilishi wa kitumaji ujumbe hiki daima ametangaza mfumo wazi kabisa wa kutengeneza pesa na kuwahakikishia watumiaji wake kutopokea matangazo ndani ya programu hiyo. Kile tu ambacho huduma hii inataka kujua ni nambari yetu ya simu. Na zaidi kidogo: uwezo wa kufikia kitambu chetu cha anwani, uwezo wa kufikia kamera, uwezo wa kufikia maikrofoni…

WhatsAppp na timu yake wamejishindia imani bila kikomo kutoka kwa watumiaji kutoka kote ulimwenguni. Inaweza kuwa ilionekana kwamba – kimetimia, kitumaji ujumbe bora zaidi. Mpaka wakati ilipofikia “ununuzi wa karne” wakati papo hapo data zetu zikapatianwa kwa mtandao wa kijamii mkubwa zaidi ulimwenguni[1]. Na ambao pia una mambo mengi zaidi yasiyohitajika. Sasa mara kwa mara Facebook inatupendekezea kuwa marafiki na watu wageni ambao inafiki kwamba ni marafiki wetu wa karibu zaidi. Na ambao hata wao wanapokea mapendekezo sawia jambo ambalo linapelekea kuwa mkanganyiko uziotabirika zaidi.

Majaribio ya watumiaji kupinga na kuomba mamlaka simamizi[2] hayajasababisha mabadiliko yoyote makubwa. Kando na kwamba Jan Kuom ameuza nusu ya hisa zake kwa Facebook katika miezi 12 ya hivi majuzi. Na ofisi ya WhatsApp ya masuala ya umma ilisema kwamba ‘inashirikiana na mamlaka zinazosimamia ulinzi wa maelezo ili kujibu maswali yake yote.

Hapa ni mifano tatu ya bidhaa ambapo tunaweza kuona jinsi ilivyo rahisi iutumia imani yetu vibaya na jinsi ambavyo hawapo tayari kukabiliana na matatizo wakati haiwasaidii kamwe.

Katika chapisho letu linalofuatia tutashiriki baadhi ya mifano mizuri ambayo kwa bahati nzuri ipo. Ni michache zaidi na kutawa na michache zaidi lakini wakati mwingine hata mtu mmoja nyanjani ni shujaa.

[1] WhatsApp itashiriki nambari yako ya simu na Facebook kwa ajili ya matangazo  \\ 25.08.2016

[2] Ufaransa imeipa WhatsApp mwezi mmoja iwe imeacha kushiriki data na Facebook \\ 19.12.2017

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Jisajili Kupokea Jarida Letu

Kitumaji Ujumbe cha Aegees cha 2018. Haki zote zimehifadhiwa.