Ujumbe wa Telegram Kwako! Tafadhali, Weka Sahihi Hapa!

Mojawapo ya vitumaji ujumbe maarufu kila mahali ni Telegram – huduma iliyosimbwa asili yake ikiwa Urusi. Umaarufu wake ulikuwa wa hakika: mwanzoni mwazilishi wa mradi huu alilazimika kutoka kutoka Urusi ambako kulingana naye alikuwa anashinikizwa. Kisha Telegram ikapata mafanikio ya papo hapo nchini Irani, ambako mara moja iliwavutia vikosi maalum. Kisha ndani ya siku mbili ilikuwa imeanza kutumiwa na watumiaji milioni 1.5 nchini India. Mafanikio haya yalihusishwa na ujumbe uliosambaa kwa Wahindi kupitia mitandao ya kijamii kwamba huduma hiyo ilikuwa na asili ya Kihindi na vitumaji ujumbe shindani.

Februari 2014: kwa ajili ya kutokuwepo kwa huduma ya WhatsApp kwa saa 1.5 huduma hii ya Durov ilipakuliwa na kusajiliwa mara milioni 1.8 ndani ya siku moja. Oktoba 2014: kitumaji ujumbe hiki kilipata umaarufu nchini Korea Kusini kwa ajili ya ujumbe kutoka kwa ofisi ya mashtaka kuhusu upelelezaji mitandao ya kijamii kuhusiana na mada ya uvumi bila msingi uliokuwa ukienea. Kisha mara mbili, mwezi Desemba 2015 na 2016 huduma hii ilianza kutumiwa nchini Brazili na kupakuliwa mara milioni 4 na 7 mtawalia, mara yote mbili watumaiji walikuwa wanahama kutoka WhatsApp ambayo ilikuwa imezuiliwa kwa muda na mamlaka za nchi hiyo.

Shughuli ya timu ya mradi mara kwa mara inaambatana na kashfa na kauli kubwa kwenye vyombo vya habari na vitendo vyote mara nyingi zinaonekana kuwa ni jambo lilikuwa limepangwa kwa makini. Wanaofuata nadharia hizi za masuala tete wanapata dhana tosha za kuwaza lakini katikati mwa yote hayo mtu anaweza kuona kwamba:

  1. Telegram ni rahisi kutumia, imetengebnezwa kwa makini na zana nzuri ya kubadilishana maelezo;
  2. Huduma hii haifichui matokeo yoyote ya kifedha isipokuwa kabla ya ICO;
  3. Kitumaji ujumbe hiki kinadai usalama lakini hakijitahidi kudhihirisha hili.

Na kitu cha mwisho kwenye orodha hii ambayo pengine inatilia shaka juhudi nyingi za timu hii za kupata sifa ya kuwa ‘kitumaji ujumbe cha kwanza kinachozingatia usimbaji kikamilifu’. Kauli hii yenye utata imewekwa vyema zaidi na Moxie Marlinspike, mwazilishi wa Signal:

            Durov anataka kubadilishana usiri ili kupata uaminifu (kwa mtu fulani)

Alielezea wazo la mwazilishi wa Telegram kwa kutumia maneno ‘bilionea anaweza kuaminika kwa sababu hawawezi wakanunulika’. Mtengenezaji huyu pia alidokeza kwamba hali ya usimbaji kwenye vifaa mtumaji na mpokeaji ujumbe ni kwamba ikiwa protikali hii inafanya kazi, kama katika tukio la Signal – watumiaji hawahitaji kumwamini mtu mwingine yeyote.

Katika tukio hili haijalishi kamwe jinsi Pavel Durov alivyojibu. Tunaona kwamba mradi huu haujafanyiwa ukaguzi wowote. Badala yake daima kuna juhudi za kutafuta mianya kwa mfumo wa ushindani na fedha za tuzo kubwa kubwa – zinavutia wengi, vyombo vya habari na kusababisha msisimuko mkubwa pia. Lakini wataalam hawaamini vitendo hivyo. Haviko hadharani na kwa hivyo haviwezi kukaguliwa.

Hilo lilikuwa tendo la kujipendekeza wakati Telegram ilikataa kufuata sheria za bunge la Urusi: hapo awali ukataaji kama huu ungepelekea kuzuiliwa kwa huduma hizo kama vile BlackBerry Messenger (BBM), LINE, Imo.im na Vchat isiyojulikana sana. Ya kwanza kwenye orodha ya “Kuzuiwa” mwezi Aprili 2017 ilikuwa programu ya kubadilishana ujumbe wa sauti inayoitwa Zello. Kampuni zote zilizoorodheshwa zilikataa kutoa data hizo kwa wakati mzuri ili zijumuishwe kwenye daftari la taifa. Mwezi Aprili, 13, 2018 mahakam ilitoa uamuzi kwamba Telegram ingezuiliwa, lakini walikosa kuizuiliwa hata baada ya kuzuilia anwani milioni 20 za IP. Kama ilivyokuwa hapo awali mmiliki wa huduma hii anaendelea kurudia kwamba hajawahi kushirikiana na vikosi maalum vya Urusi au Kigeni na hatawahi kushirikiana navyo.

Msimamo wa mameneja wakuu wa mradi huu hauonekani kuwa bila dosari kwamni mtu anaweza kuamini kulingana na taarifa za vyombo vya habari: kitumaji ujumbe hiki kinaendelea kuzuilia chaneli na makundi baada ya kuombwa na wawakilishi wa nchi mbalimbali. Maudhui ya maobi haya hayafichuliwi, wala kujulikana jinsi maamuzi ya kuzuilia yailivyokuwa yakifanywa. Maelezo kama haya, yanayoweka doa kwenye taswira ya bidhaa kwa kawaida yanafunikwa kwa vijisababu vizuri ili kubadilisha mawazo ya watumiaji lengwa. Na mkakati huo unadhihirika kuwa fanisi kwa ujumla.

Watumiaji wa kitumaji ujumbe wanaongezeka bila kikomo, ingawa ‘kwenye mvunguni’ bado kuna historia wazi sana katika hifadhidata za simu maizi, kama ilivyo na viongozi wote katika sekta.

 

KIUNGO KUELEKEA KWENYE VIDEO YA TATU

Hakuna njia yoyote maalum ya usimbaji katika Telegram. Badala yake inabadilishwa kwa mafanikio kwa kutumia matangazo kuhusu protokali inayoaminika zaidi na usimbaji wa ngazi ya juu. Mafanikio ya Telegram yanaungwa mkono na uchangishaji fedha wa hivi majuzi ambapo wakati wa uuzaji wa awali mradi huu uliweza kuchangisha dola milioni 850 kutoka kwa baadhi ya wawekezaji wakubwa, ikijumuisha Sequoia Capital na Benchmark. Wakati wa awamu inayofuatia ambayo imetaganzwa kupitia ujumbe wa siri kiwango jumla cha fedha zitakazochangishwa kitalinganishwa na uuzaji wa awali wa kwanza.

Mfano mzuri wa kampeni ya PR yenye mazao unaweza kuwa kwamba maelezo kuhusu ICO iliyopangwa, rekodi za mradi na matangazo ya uuzaji wa awali hayakupokea hata thibitisho moja la umma kutoka kwa wawakilishi rasmi wa Telegram. Watumiaji walijua kwamba uuzaji wa awali ulifanyika mwezi Februari, 2018 wakati Pavel Durov alifahamisha Tume ya Uuzaji wa Hisa (Marekani) kuhusu fedha zilizochangishwa.

Hata hivyo, kuna wale waliokataa kuwekeza katika kitumaji ujumbe hiki. Miongoni mwao: Pantera Capital, mojawapo ya kampuni za kwanza zilizoanza kuwekeza katika sarafu za digitali. Mshirika wake wa utafiti Charles Noyes alichambua ICO iliyopangwa na kutoa maoni yenye pingamizi:

Wanapoifanya kwa njia hii – yaani kwa njia fiche, kwa siri bila ukaguzi wa wataalam, kuna nafasi ya kufanya kosa mwanzoni kabisa. Linaweza kuwa kosa ndogo lakini linaweza kuharibu kampuni nzima.

Wakati wa ujumbe wa telegramu za makaratasi ili kutumwa ujumbe ulichapwa kwenye kipande cha karatasi na kuwasilishwa kwa anwani kwa njia wazi. Ilidaiwa kwamba wakati wa kuwasilisha hakuna mfanyikazi angesoma maudhui ya ujumbe huo. Lakini katika hali halisia mambo yalifanyika tofauti. Kwa hivyo polepole telegramu zikaanza kutumika tu kwa ujumbe wa pongezi na ilani za kifo. Baadaye, zikatokomea kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Jisajili Kupokea Jarida Letu

Kitumaji Ujumbe cha Aegees cha 2018. Haki zote zimehifadhiwa.