Tunahitaji Aina Ipi ya Kitumaji Ujum-be?

Chambuzi za hadithi nyingi za mafanikio na kutofanikiwa, data za utafiti na mapendeleo ya watumiaji zinatupelekea kwenye hitimisho zifuatazo kuhusu jinsi kitumaji ujumbe kinapswa kuwa:

  • rahisi kutumia;
  • haraka;
  • aminifu;
  • kufanya kazi;
  • kutumika katika mifumo mingi tofauti.

Viongozi wote kwa kiwango kikubwa au kidogo wanatimiza mahitaji haya:

Tukitenga baadhi ya miradi ya kitaifa na mtandao wa kijamii wa Snapchat kutoka kwenye orodha hii tunafikia tano bora: WhatsApp; Facebook Messenger; Skype, Viber; Telegram.

Mara moja tunatambua kwamba huduma tatu za kwamza zinatumia protokali ya Signal. Utekelezaji wake unastahili kuaminika, kuna matokeo ya ukaguzi yanayopatikana[1], hakuna mifano inayojulikana ya mashambulizi yaliyofanikiwa.

Viber hutumia protokali yake binafsi iliyo na msingi kwenye teknolojia sawia ya Double Ratchet, lakini tofauti Signal, protokali ya Viber imeandikwa kutoka mwanzo. Telegramu inatumia protokali yake binafsi asilia. Vitumaji ujumbe hivi viwili pia vinaweza kuchukuliwa kuwa vimesimbwa tunapozungumzia masuala ya kiufundi.

Hebu turejee kwenye mahitaji yaliyoorodheshwa hapa juu.

Tukiangazia urahisi wa kutumia tunachagua Telegram na WhatsApp.

Zilizo za haraka zaidi ni Telegram na WhatsApp. Pia ndizo zinazotumika sana zaidi.

Telegram na WhatsApp zinarekebisha matatizo yao sugu kwa haraka.

Kutumika katika mifumo mingi tofauti — zote zinatumiza isipokuwa Facebook Messenger (haina toleo la kompyuta).

Na swali kuu linaloulizwa na mtumiaji wa kawaida, hebu tuseme ‘mama wa nyumba’: ni wapi ninaweza kupata wasiliani wangu wengi zaidi? Viongozi wazi hapa ni Facebook Messenger na WhatsApp pamoja na masoko ya India na Brazili. Tofauti tu ni China ambapo uongozi unashikiliwa na huduma za kitaifa za WeChat na QQ.

Hebu tujikumbushe ni vitumaji ujumbe vipi vinashirikiana na serikali na vinafanya hivyo kwa njia ipi. Kulingana na data kutoka kwa vyanzo wazi vya tunajifunza yafuatayo: Skype na Viber walikuwa wanapatiana data baada ya kupokea maombi kutoka kwa mashirika maalum bila ya maamuzi yoyote ya mahakama. Facebook Messenger, Telegram na WhatsApp hawakufanya hivyo. Hata hivyo Telegram ilikuwa inapata maoni mabaya kutoka kwa watumiaji wake baada ya kufunga makundi na chaneli baada ya kuombwa na serikali na bila ya maamuzi yoyote ya mahakama.

Bila kutaka sifa na baada ya hata kufanya uchambuzi huu hali ya juu kuhusu 5 BORA tunasalia na kiongozi mmoja tu na wa pekee: WhatsApp (ikijumuisha vijisababu kadhaa kwa sababu ya utengenezaji majukwaa ya kutumika katika mifumo mbalimbali, hatari za watumaji ujumbe taka na kushughulika na faili).

Tukizingatia kwamba huduma hii haihifadhi data za watumiaji na kwa hivyo haiwezi kuzipatiana baada ya kumbwa na mtu (jambo ambalo lilidhihirishwa vyema sana wakati wa mgogoro wake na mamlaka za Brazili) – tokeo la Jan Kuom ndicho kile ambacho mtumiaji anahitaji leo.

Hata hivyo, huu ni upande mmoja tu wa sarafu moja. Ni nini kinatendekea maelezo yaliyohifadhiwa kwenye vifaa vya mtumiaji? Kuna sheria zipi katika kutengeneza hifadhirudufu za mtumiaji, zinahamishwa vipi, na kuhifadhiwa wapi? Huduma hii inaweza kukataa mashambulizi ya aina mbalimbali? Na kuhusu milango ya nyuma tena, ile ambayo vyombo vikuu ya habari ulimwenguni viliangazia katika machapisho yao[2]?

Unaweza kujua katika makala yanayofuatia.

[1] Uchambuzi Rasmi wa Usalama wa Protokali ya Kutuma/Kupokea Ujumbe ya Signal \\ kufikia Novemba, 2017

[2] Kipengele cha muundo wa WhatsApp inamaanisha kwamba baadhi ya ujumbe uliosimbwa unaweza kusomwa na mhusika mweingine \\ kufikia Januari, 13 2017

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Jisajili Kupokea Jarida Letu

Kitumaji Ujumbe cha Aegees cha 2018. Haki zote zimehifadhiwa.