Ni nani anayeihitaji?

Kuna maoni pana kuhusu mahitaji makubwa ya mbinu salama za mawasiliano kati ya wawakilishi wa miundo ya jinai au washiriki katika mashirika ya kigaidi. Swali hili ni gumu kuuliza wakati hauna takwimu zozote tayari, kwa hivyo hebu tu tuendelee na dhana.

Dhana msingi inaweza kuwa kama ifuatavyo: hakuna ukweli hata mmoja unaohakikisha ukuaji wa uhalifu uliopangwa na ugaidi unaosababishwa na matumizi ya vitumaji ujumbe. Lakini kuna taarifa zinazothibitisha kwamba mbinu hizo za mawasiliano ya dijitali zinasaidia kuzuia shughuli haramu. Hivi karibuni tu kulikuwa na hadithi kuhusu kudakizwa kwa shirika kubwa la kimataifa la biashara ya madawa ya kulevya ambalo lilikuwa linatumia kitumaji ujumbe kilichosimbwa kwa kutumia simu maizi ya kipekee iliyosimbwa ili kupanga shughuli zake. Kifaa hiki kilichotengenezwa kwa maombi hakikuwa na maikrofoni, kamera na hata kivinjari. Utendaji pekee uliopatikana kwenye kifaa hiki ulikuwa mazunguzo kwa maandishi ya siri.

Haikusaidia. Kando na washiriki wa kundi haramu polisi walimkamata mmiliki biashara hiyo ya kutengeneza vifaa vya watumiaji ambaye, kulingana na mashirika ya kutekeleza sheria alikuwa anashiriki katika shughuli za kundi hilo.

Dhana nyingine msingi: vitumaji ujumbe husaidia kupigana na jinai kwa njia fanisi zaidi kwani afisa anayetekeleza jukumu lake kwa kuficha utambulisho wake anaweza kwa urahisi zaidi anaweza kupenyeza kwenye kundi la uhalifu bila kujulikana – tusema kwa kuchukua kifaa cha mwanachama amilifu wa kundi hilo kwa ruhusa yake au bila ruhusa yake. Hatari ndogo zaidi na kupata maelezo mengi zaidi ndani ya muda mchache.

Na bila shaka, mawakala wa kutekeleza sheria wanajua gharama ya kutofaulu huku na pia wawakilishi wa ulimwengu wa jinai. Na ndio sababu makundi ya uhalifu hufanya maamuzi makubwa zaidi wakiwa nje ya mtandao. Na maamuzi makuu ya jinai yanasafirishwa kwa njia za jadi jambao ambalo halijabadilika kwa zaidi ya miaka mia moja. Tunaweza kuchukua tokeo hili kama dhana nyingine lakini linaonekana zaidi kuwa jambo la kweli.

Boko Harama wala Taliban hawalalamiki kwamba hakuna intaneti na vitumaji ujumbe katika maeneo ambayo yanasimamiwa kikamilifu na makundi haya ya kigaidi. Upeo wa uzalishaji heroine katika pembetatu ya Dhahabu (Golden triangle) mwishoni mwa karne iliyopita wakati ujumbe wa siri ulikuwa unaandikwa kwa kutumia maziwa kwenye karatasi ya papyrus. Kolombia ilikuja kuwa mzalishaji mkuu wa kokeni wakati wa kitumaji ujumbe cha kwanza – na matukio haya mawili hayahusiani kamwe.

Kwa hivyo, ni nani anayetaka usiri katika mawasiliano ya mtandaoni?

Kwanza kabisa, ni wale wanoishi ndani ya mifumo ya dini kali na vikwazo vya kikabila. Inaweza kuonekana kuwa jambo la kushangaza lakini baadhi ya nchi zilizo na utamanduni duni wa kisheria tayari zina intaneti ya broadband na ujumbe usio wa heshima ukitumwa kwa mwasiliani asiyestahihili – na mwanamke aliyeoleka ambaye ana tabia nzuri unaweza kuuawa hadharani katikati mwa jiji. Hii ni halisi na hitaji la mbinu zilizosimbwa za mawasiliano kwa wananchi wa dini kama hizi ni jambo halisi pia.

Uhalisia ni idadi ya vita vya ndani kwa ndanio na migogoro ya kikabila ambapo jamii inagawanywa kuwa ‘yetu’ na ‘yao’ kwa njia isiyotabirika kabisa. Na ambapo gharama ya neno iko juu sana. Kufupisha mambo ndipo ni muhimu zaidi.

Uhalisia ni kuendesha biashara katika nchi zinazoendelea ambako masoko na kanuni ni wakati zinaanza kuundwa. Katika maeneo ambako milionea anapopoteza simu yake maizi anapoteza bishara wakati kwa wakati huo.

Mifano kama hii inapatikana kwa wingi.

Hata hivyo, tukijaribu kuchungulia siku za usoni tunaweza kugundua mtindo ambao haujajithihirisha wazi ambao kwa sasa unaweza kuitwa ‘hitaji la nafasi ya kibinafsi’. Leo ustaarabu wetu unaanza kuwaza kuhusu haki ya kila mwanadamu ya kukataza hadithi geni ya kitabia; hali ya kwenda kinyume na jamii; haki ya kuishi maisha mawili, jameni! Au angalau kuwa na maisha bila matangazo.

Sehemu maizi ya mwanadamu ni kujitahidi ili kupata ubinafsi na kuupata. Wengine hata hawawezi kunusurika.

Hawa wa kwanza wanahitaji vitumaji ujumbe vilivyosimbwa

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Jisajili Kupokea Jarida Letu

Kitumaji Ujumbe cha Aegees cha 2018. Haki zote zimehifadhiwa.