Data — kwa bei yoyote

Chapisho hili linaanzisha msururu wa machapisho kuhusu usalama wa kitumaji ujumbe – wa kimafikira na halisia. Hebu tujaribu kujua jinsi data yatu imelindwa katika matukio yote mawili kuanzia mambo rahisi hadi yale magumu.

Si siri kwamba kampuni zingependa upata data zetu za kibinafsi. Hebu tutazame mwaka 2017 wakati hitaji la kujua mapendeleo ya watumiaji liliongezeka maradufu na pia kampuni kugharimika kwa kununua maelezo hayo. Hata mmiliki duka la pizza angependa kujua un-apendelea aina ipi ya jibini: ikiwa unapenda mozarella mbona atumie parmesan ambayo ni gali zaidi?

Tofauti na pizzeria ambapo ninaweza kuulizwa kuhusu mapendeleo yangu, kampuni ha-wapotezi muda wao wa kitaka kujua na kuwasiliana na wateja wao. Wanatulazimisha tushiriki maelezo yetu ya kinafsi pamoja nao au wanayapata kwa njia zao wenyewe, na kutu-fahamisha tu kwa kiwango fulani. Na hapa ndipo tunapokumbana na mtu mbaya, na kama mwandishi mmoja wa jadi alivyosema, the devil is always in the details.

“Kiwango fulani” inamaanisha maandishi madogo yanayoonyeshwa kwenye kidirisha kinachotokea ambacho hakionekani vyema miongoni makubaliano ya mteja ya kurasa 120, au wauzaji na wachambuaji wengi wachezaji shere. Michezo hii ya shere yamekuwa ya ka-waida kiasi kwamba hatuitamvui tena. Maelezo yanayotuhusu yanageuka kuwa bidhaa inayouzwa na mtu mwingine isipokuwa sisi.

Suala moja la kushangaza na ambalo halijulikani sana linazungumzia jinsi tabia ya mtumiaji inavyoweza kuwa muhimu. Miaka michache iliyopita jukwaa la utafitaji la Google liliondoa kwenye matokeo yake ya utafutaji kitu chochote kinachotaja kampuni ndogo inayoitwa Ad Nauseam ambayo iliwaomba watumiaji kusakinisha ungani wa kivinjari wavuti. Utendaji pekee wa ungani huu ulikuwa kusababisha ubonyezaji bila mpangilio wa matangazo yaliyo-tokea kwenye ukurasa wowote. Dhana hii haikuwa imeendelezwa sana, lakini ilitishia sana uwezo wa Google wa kutengenza sifa nzuri kwa watumiaji, jambo ambalo lingesababisha uharibifu mbaya sana kwenye soko la matangazo ya dijitali. Google iliona hili mara moja na huduma hiyo inatangazwa kuwa si halali.

Kujua data zetu za kibinafsi ni biashara kubwa na yenye mapato. huu ni upande mmoja wa suala hili. Upande mwingine ni kwamba maarifa haya ni zana ya kututumia sisi. Na kwa kweli hatujui ni gani mbaya kuliko ile nyingine. Kwa kweli jambo moja oinaweza kusemwa: mtumiaji ana haki ya kuchagua ni nini cha kushiriki na ni nani wa kushirikisha naye. Na cha-guo lake ni lazima litambuliwe kadri iwezekanavyo.

Mtu anaweza kusema kwa kweli kwamba mawasiliano ya wanadamu inatiririka kutoka kwenye mitandao ya kijamii hadi ndani ya vitumaji ujumbe, lakini hata kwa njia hii kuna mambo yasiyojulikana ambayo yanawatarajia. Na hivyo matangazo yanayoudhi na pia jum-be za Facebook zisizohitajika zilizojificha kwenye matangazo zinawahamasisha watumiaji kuhamishia mazungumzo kwenye Facebook Messenger. Hata hivyo, mtu anapogundua kwamba hilo halikuepushani na wauzaji mtu anahamia WhatsApp. Wakati mchakato huu wa watumiaji kuhama unafikia kiwango cha juu kupindukia Mark Zuckerberg ananunua WhatsApp. Anainunua kwa kiwango cha kushangaza cha dola bilioni 19. Hiyo ndiyo bei ya kampuni ambayo mapato yake ya kila mwaka ni dola milioni 20!

Kwa mtazamo wa kwanza kiwango cha fedha kinaonekana kuwa cha kustaajabisha lakini tukigawa fedha hili kwa milioni 450 (hii ndio idadi ya watu waliojisajili na WhatsApp mnamo ilipouzwa) basi tunaona kwamba bei ya data za kibinafsi za kila mtumiaji ni dola 42 pekee.

Dola arobaini na mbili kwa data nyingi kukuhusu wewe na orodha ya wasiliani wako – je, kwa kweli hii ndio bei ya maelezo kuhusu maisha yako?

Uko tayari kushirikisha data zako na kampuni na kuziruhusu kutengeneza pesa wakikutumia?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Jisajili Kupokea Jarida Letu

Kitumaji Ujumbe cha Aegees cha 2018. Haki zote zimehifadhiwa.